
Kama vile ambavyo kuna siri katika kupata utajiri,kuwa na ndoa bora;vivyo hivyo kuna siri kubwa iliyojificha katika vitabu.
Jamii imekuwa na mwamko mdogo wa usomaji wa vitabu kwa sababu kadha wa kadha.Lakini sababu mojawapo ambayo inachagiza jamii isiwe na mwamko wa kusoma vitabu imejikita katika tamaduni.
Tamaduni zetu zimeathiri usomaji wa vitabu kuwa duni,Hii inatokana jamii imejikita kushugulika na shughuli za kijamii zaidi kama vile kulima ,kucheza ngoma n.k.
Tunaona asilimia kubwa ya wateja wengi wa maktaba zetu ni wanafunzi na wanavyuo , pia inatoka na kundi hili wanasoma vitabu iwasaidie katika kujibia mitihani yao.
Kwa nini vitabu vimebeba siri?
Kwanza, Kitabu kinafanya msomaji kuwa mbunifu na kupata maarifa mengi yatakayomsaidia kufikia katika maendeleo ya hali ya juu.Kwa hiyo tunaweza kusema kuna faida kubwa kwa jamii kujijengea tabia ya kusoma vitabu ni chanzo cha kupata maendeleo.
Pili,Kitabu kinasaidia kujenga jamii inayo heshimu haki za binadamu.Tunaona kwa sasa nchi nyingi zinapambana na raia wake kuheshimu haki za binadamu.Nahamini kupitia siri iliyojificha kwenye kitabu itasaidia jamii kuwa utu na kuwajali watu wengine itapunguza visa vinavyotokea vya uvunjifu wa haki za binadamu.
Naomba nihitimishe makala hii kwa kuwahimiza wanajamii kujenga tabia ya kusoma vitabu ili kusaidia jamii zetu ikue kimaendeleo.
Jackson C. Chacha
Lushoto,Tanzania
22/10/2019