Awali ya yote nitumie ukurasa huu kuwashukuru nyote mnaopitia ukurasa huu kwa ajili ya kujifunza na kupata elimu zinazohusu huduma za Maktaba.karibu sana.
Naomba nianze moja kwa moja kwa kuleta ufafanuzi wa mada tajwa hapo juu.
MKUTUBI ni Nani?
Kwa kweli hili neno linaweza kuwa geni masikioni mwa watu wengi ila ndiyo ukuaji wa kiswahili ulivyo ila itoshe kusema Mkutubi ni mtu mwenye weledi wa taaluma ya maktaba na kazi yake kubwa ni kuweka mpangilio mzuri wa machapisho yote yaliyopo ndani ya maktaba ili kumrahisishia msomaji kupata machapisho kwa urahisi.
Baada ya kufahamu dhana nzima ya neno "Mkutubi" tuangalie lengo la mada yetu.
Kwa ujumla maktaba ni mkusanyiko wa machapisho mbalimbali yaliyopangiliwa kwa usahihi kumrahisishia msomaji aweze kupata hitaji lake kwa muda sahihi.
Maktaba haiwezi kukamilisha kazi zake bila kuwepo Mkutubi aliyepata mafunzo/elimu ya kutosha ya kiukutubi ,ambayo itaweza kukamilisha maana nzima ya uwepo wa huduma ya maktaba.
Jamii ina wajibu wa kuelewa huduma za maktaba ili kuwa na taifa lenye watu walioelemika,hivyo ni jukumu la serikali kuongeza nguvu zaidi kwenye kujenga miundombinu ya kutosha hasa sehemu za pembezoni zizofikika huduma za maktaba kupanua wigo kwa jamii kuelimika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni