Jumapili, 15 Januari 2017

KUMJENGEA MTOTO KUWA NA TABIA YA USOMAJI WA VITABU

Usomaji wa vitabu kwa nyakati hizi hauwezi kukwepeka hasa katika ulimwengu huu unaolekea kwenye mapinduzi makubwa ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.
'' Shirika la UNESCO linasema utamaduni wa kujisomea vitabu unazidi kupungua duniani. Tanzania ilifikia kiwango cha juu zaidi cha usomaji wa vitabu katika miaka ya 70.''
Tamaduni hii ya usomaji wa vitabu hasa kwa jamii za Kiafrika umekuwa duni sababu ikiwa ni mifumo tuliorithi kutoka kwa wakoloni lakini sababu hizi zisiwe kikwazo za jamii kutosoma vitabu.
Tabia ya kumjengea mtoto kuwa na mazoea ya kusoma vitabu ni njia muhimu sana itakayomsaidia mtoto kuwa na ukuaji ulio bora.
Kwa sasa najua sio tatizo tena kwa wazazi kusoma vitabu vyenye kuleta tija ya maendeleo.

Hatua za kufuata katika kumjengea mtoto tabia za usomaji vitabu
  • Mzazi kuwa mfano wa kuigwa katika kusoma kitabu... weka utaratibu maalumu kwa familia kuwa na programu ya kusoma vitabu.
  • Msaidie mtoto kusoma kitabu hasa sehemu zenye kuleta utata.(zingatia umri na uelewa wa mtoto)
  • Mwekee mtoto utaratibu mzuri wa kusoma kitabu na kuwasilisha taarifa fupi mara amalizapo.
  • Jenga utaratibu wa kumnunulia vitabu mbalimbali hasa vitabu vinavyochochea maarifa kwako na mtoto.
  • Mpongeze mtoto anapoonesha juhudi ya kusoma (Chagua zawadi zinazochochea usomaji)  

         
Hongera sana kwa kutimiza zoezi hili
Soma vitabu upate maarifa kwa sababu maarifa mengi yamefichwa


Kwa maoni na mawasiliano
Clement,Jackson
Librarian - The university of Dodoma (UDOM)
E-mail:jackson.clement81@yahoo.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni