Jumamosi, 13 Mei 2023

MAKTABA MTANDAO

 Maktaba mtandao linaweza kuwa jina geni kwa baadhi yetu,lakini tusishangazwe na jina unajua kiswahili ni lugha pana sana hasa kwa dhama hizi za ukuaji wa Sayansi na Teknolojia.

Maktaba Mtandao ni neno ambalo limetafsiriwa kutoka lugha ya kiingereza likiwa na maana ya "digital library".

Nini maana ya Maktaba Mtandao?

Maktaba Mtandao ni mkusanyika wa machapisho mbalimbali yaliyopangwa kwa mifumo maalumu na kuhifadhiwa kwenye kompyuta na watu wanayapata kupitia mtandao.

Teknolojia ya habari na mawasiliano imeleta mapinduzi ya hali ya juu katika utoaji wa huduma za maktaba.

Kwa sasa mtumiaji wa maktaba haitaji kutembelea maktaba moja kwa moja kuonana na wakutubi kwa ajili ya kupata machapisho.Huduma ya maktaba mtandaoni itamsaidia kupata machapisho mahali popote na kwa Muda wowote atakapohitaji huduma ya machapisho.

Katika kupata huduma hiyo ni muhimu mtumiaji wa maktaba kuwa na kompyuta na kifaa cha kuruhusu kupata huduma ya mtandao.Iwapo hauna vifaa hivyo ni vizuri ukatembelea ofisi za Posta au mahali penye huduma ya mtandao(Internet cafe shop)


Jackson Chacha

Mkutubi- Chuo cha Uongozi wa  Mahakama 

Email:jackson.chacha@ija.ac.tz


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni