Inavyoelekea kwa sasa amani yetu imeanza kupotea kutokana na mfululizo wa matukio ya uharifu ikiwamo kuvamiwa vituo vya polisi,kuuawa kwa polisi na jingine kubwa la juzi la mapigano baina ya polisi wakisaidiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) dhidi ya makundi yanayodhaniwa kuwa ni ya kigaidi au ujambazi.
Matukio hayo yanafanya Taifa kuwa katika wasiwasi hasa kwa kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba na kura ya maoni ya katiba pendekezwa.
Tukio la Tanga
hivi karibuni kumetokea mfululizo wa milio ya risasi zikirindima maeneo ya Tanga kwa zaidi ya saa 48.
Katika mapambano hayo ,askari mmoja wa JWTZ alipoteza maisha na wengine wapiganaji zaidi ya sita wakijeruhiwa.
Mpaka tunaandaa taarifa hii hakukuwa na taarifa ndani ya jeshi kuhusiana operesheni hiyo.
Mbali na kutokamatwa kwa watu hao ambao hawajulikani ni waalifu wa aina gani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni