Intaneti ni nini?
ni mfumo wa kushirikiana kwa kompyuta unaowezesha kompyuta mbalimbali duniani kuwasiliana kati zao. Kupitia mtandao huu, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe. Ni ile mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta (kama google) au kwa kamusi kama wikipedia.
Intaneti ni mfumo wa ulimwengu wa mitandao ya kompyuta inayotumia Itifaki inayokubalika ya intanet Suite (TCP / IP) kutumikia mabilioni ya watumiaji duniani kote. Ni mtandao wa mitandao ambayo ina mamilioni ya mitandao binafsi, mitandao ya umma, mitandao ya kielimu, mitandao ya biashara, na mitandao ya serikali zenye upana wa kimitaa na kiulimwengu ambazo zimeunganishwa na safu pana ya teknolijia za mtandao za elektroniki na za mwangaza.
Intanet hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za Mtandao wa ulimwengu nzima (WWW) na miundombinu ya kusaidia barua pepe. Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za simu na televisheni, zimeundwa upya kutumia teknolojia za intanet, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia intanet (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika Tovuti, ubadilishaji maoni, na kupatiana habari zinapotokea. Intanet imewezesha au kuharakisha uumbaji wa aina mpya za mwingiliano za kibinadamu kupitia ujumbe wa moja kwa moja, jukwaa za Intanet na tovuti za kijamii.
Asili ya mtandao ina mizizi katika mwongo wa 1960 wakati Marekani ilifadhili miradi ya utafiti wa wakala zake za kijeshi na kujenga mitandao iliyosambaa ya kompyuta ambazo zina uwezo wa kustahimili mabadiliko na ni vumilivu kwa makosa. Kipindi hiki cha Utafiti na ufadhili wa raia wa Marekani wa uti mpya wa mgongo uliyofanywa na msingi wa kitaifa wa sayansi ulisababisha dunia yote kushiriki katika maendeleo ya teknolojia mpya na ukasababisha ufanya biashara wa mtandao wa kimataifa katikati ya mwongo wa 1990, na kusababisha kujulikana kwa zana nyingi katika karibu kila nyanja ya maisha ya kisasa ya binadamu. Kufikia mwaka wa 2009, wastani wa robo ya idadi ya watu duniani hutumia huduma ya Intanet. Intanet haina utawala wa kati katika utekelezaji wa kiteknolojia au sera ya upatikanaji na matumizi; kila mtandao jumuishi unaweka masharti yake yenyewe. Ufafanuzi tu wa jina mbili kuu katika Intanet, Itifaki ya anwani za Intanet na mfumo wa makundi ya majina, ndizo zinazongozwa na shirika iliyoagizwa ya, Ushirika wa kupeana majina na nambari za intaneti(ICANN).
Msingi wa kiteknolojia na masharti ya itifaki misingi (IPv4 na IPv6) ni shughuli ya kikundi maalum kilichoundwa kutekeleza kazi za uhandisi wa intanet (IETF), ambalo ni shirika la kimataifa lisilo la kutengeza faida ambalo washiriki wanaweza kuhusika nalo kwa kutoa mchango wa kitaalamu.
Kwa msaada wa mtandao
Imetayarishwa na,
CHACHA,J.Clement
Librarian-The University of Dodoma
Email-jacksonclement73@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni