Jumatano, 16 Desemba 2015

LIBRARY AND SOCIETY-1

A library is a collection of sources of information and similar resources, made accessible to a defined community for reference or borrowing.[1] It provides physical or digital access to material, and may be a physical building or room, or a virtual space, or both.[2] A library's collection can include books, periodicals, newspapers, manuscripts, films, maps, prints, documents, microform, CDs, cassettes, videotapes, DVDs, Blu-ray Discs, e-books, audiobooks, databases, and other formats. Libraries range in size from a few shelves of books to several million items. In Latin and Greek, the idea of bookcase is represented by Bibliotheca and Bibliothēkē (Greek: βιβλιοθήκη): derivatives of these mean library in many modern languages, e.g. French bibliothèque. The first libraries consisted of archives of the earliest form of writing—the clay tablets in cuneiform script discovered in Sumer, some dating back to 2600 BC. Private or personal libraries made up of written books appeared in classical Greece in the 5th century BC. In the 6th century, at the very close of the Classical period, the great libraries of the Mediterranean world remained those of Constantinople and Alexandria. A library is organized for use and maintained by a public body, an institution, a corporation, or a private individual. Public and institutional collections and services may be intended for use by people who choose not to—or cannot afford to—purchase an extensive collection themselves, who need material no individual can reasonably be expected to have, or who require professional assistance with their research. In addition to providing materials, libraries also provide the services of librarians who are experts at finding and organizing information and at interpreting information needs. Libraries often provide quiet areas for studying, and they also often offer common areas to facilitate group study and collaboration. Libraries often provide public facilities for access to their electronic resources and the Internet. Modern libraries are increasingly being redefined as places to get unrestricted access to information in many formats and from many sources. They are extending services beyond the physical walls of a building, by providing material accessible by electronic means, and by providing the assistance of librarians in navigating and analyzing very large amounts of information with a variety of digital tools.

Jumatatu, 16 Machi 2015

Ongezeko la picha za watoto mitandaoni siyo sahihi

Maendeleo ni matokeo ya jitihada na nguvu zilizotumika katika kuwekeza. Taifa haliwezi kupata maendeleo ya kweli mpaka pale thamani ya watoto wake inapowekwa wazi kwa kila raia.

Mtoto ni rasilimali ambayo ikiandaliwa vyema taifa linaweza kufikia maendeleo na kuondokana na umasikini. Familia, jamii na taifa kwa ujumla tuna wajibu wa kutambua thamani ya watoto, kuwathamini, kuwalinda na kuwapatia haki zao kama elimu. Kufanya hivyo kutakuza vipaji vyao ambavyo baadaye vitakua taaluma.

Jinsi utandawazi unavyozidi kuenea, tumekuwa tukizidi kuona picha za watato wadogo mitandaoni wakiwa watupu bila nguo, wengine wameshika chupa za pombe kana kwamba wanakunywa na wengine wakivuta sigara.Je, hizi picha zinawapa watoto ujumbe gani?

Kama mtoto akifanya kosa mzazi unampiga picha badala ya kumuelekeza, unamfundisha nini? Inakera sana kuona ongezeko la usambazaji wa picha na video za watoto wadogo wakiwa uchi wakifanya ngono.

Jamii itambue kuwa ni kosa la jinai kisheria kurekodi mtoto katika hali yoyote bila idhini ya mzazi au mlezi wake. Vilevile ni kosa la kimaadili na kitaaluma (kwa mpiga picha) kuweka video ya mtoto akiwa mtupu bila kuficha sura yake kwa ajili ya kumlinda mtoto huyu. Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 inatamka wazi kwamba ‘Mtu hatachapisha, kutengeneza, kuonyesha au kuagiza kuchapishwa, kuendeshwa au kuonyeshwa picha au taswira ya mtoto au mtoto aliyefariki, inayoonyesha ukatili au katika pozi za ngono.’ Sheria inatamka kwamba yeyote atakayekiuka masharti ya maelekezo ya kutopiga ama kuchapisha picha za mtoto kama ilivyoelezwa hapo juu, anatenda kosa la jinai na atakapotiwa hatiani atalipa faini isiyopungua shilingi laki tano au kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja. Ama kwa kujua au kutokujua, jamii hukiuka sheria hii mara nyingi.

Picha hizi hudhalilisha watoto, familia zao na hata kuwaathiri kisaikolojia watoto wenyewe na rafiki zao ambao pia ni watoto.

Haziwasaidii kwa namna yeyote zaidi ya kuharibu heshima na utu wa watoto hawa na kudhoofisha ukuaji na maendeleo yao. Watoto ni kama vioo, wanaakisi kile wanachokiona mbele yao. Wahalifu katika kupiga na kusambaza picha za watoto mitandaoni ni jamii nzima hasa wanaochekelea wakipata picha hizi na wenye mshawawa wa kuzisambaza kwenye makundi yao mitandaoni. Wengine ni wamiliki wa vibanda vya filamu mtaani, maarufu kama ‘vibanda umiza’. Hawa wanaonyesha filamu za aina zote bila kujali umri wa wateja wao. Watoto wadogo wanaruhusiwa kuingia kuona filamu za ngono alimuradi wanazo pesa za kiingilio. Ingawa mzazi huwezi kuwa kila mahala alipo mwanao. Kama jamii na taifa kwa ujumla tunao wajibu wa kuhakikisha tunawakinga watoto na mambo yanayoweza kuhafifisha ukuaji wa vipaji vyao na maendeleo yao.

Ili tuweze kuwekeza kupitia watoto hawana budi kuheshimiwa utu wao. Ni jukumu la jamii nzima kuepuka kusambaza picha za watoto zinazodhalilisha utu wao, jambo ambalo limeenea sana hasa katika mitandao ya kijamii. Kufanya hivyo kunaweza waathiri kisaikolojia, jambo linalodumaza maendeleo yao hata wanapokua watu wazima. Kama jamii na taifa kwa ujumla hatuna budi kuwawekea mazingira mazuri watoto yatakayo imarisha afya zao kimwili na kiakili ili kuandaa taifa la kizalendo litakalowajibika kikamilifu kukua kimaendeleo toka ngazi ya kaya hadi taifa. Wote kwa pamoja hatuna budi kuwapongeza pale wanapofanya vizuri, kuwatia moyo pale wanapokata tamaa kufanya jambo fulani na kuwaelekeza kwa upendo pale wanapokosea na si kuwapiga picha na kuchekelea makosa yao na rafiki zetu.

Makala haya yameandaliwa na wataalamu wa makuzi toka Sema

Source:http://www.mwananchi.co.tz

Jumanne, 10 Machi 2015

TEKNOLOJIA YA KISASA YA UKUSANYAJI WA TAARIFA KUTOKA KAMPUNI YA PUSH OBSERVER

Push Observer Limited ni kampuni ya Tanzania inayomiliki vyombo vya kiinteligencia na teknolojia ya sanaa ya kufuatilia, kukamata na kuchuja vyombo vya habari -magazeti, matangazo (radio & televisheni), Internet na uchambuzi, ripoti ya ushindani kwa ajili ya biashara, serikali na wateja wengineo wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Hivi sasa, Push Observer wanachunguza vituo vya redio 90+, vituo vya televisheni 15+, magazeti (magazeti, majarida, magazeti na majarida) 70+ na machapisho online ikiwa ni pamoja na blogs na mitandao maudhui.

Observer ni kampuni ya kiTanzania inayoongoza kidigitali, kwa viwango vya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa katika data na uanachama na vyombo kama FIBEP, Nudge, Vision Critical, na Harvard Innovation Labs. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mikakati wa Six Telecoms, Kampuni mama ya Push Observer, Rashid Shamte alisema kuwa kupitia teknologia hii ya usambazaji ya kisasa, wateja wao wataweza kupata habari taarifa muhimu na mpya masaa ishirini na nne ya wiki.

Aliongeza kuwa,tumezindua teknolojia hii kwa wateja wetu kutokana na teknologia ya uchunguzi wa vyombo vya habari kubadilika sana miaka ya karibuni”. “Huduma hii ya kusambaza taarifa imekuwa ya kisasa, rahisi na ya ubora wa hali ya juu kutokana na uwekezaji wetu katika teknolojia hii. Wana vifaa vya kisasa ambavyo vinaweza kupata taarifa kupitia televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na redio kwa muda muafaka, vifaa hivyo vinauwezo wa kupata taarifa had 350,000 kutoka vyombo mbali mbali. Kwa kutambua mahitaji ya wateja wetu kupata habari na taarifa za muhimu tumeamua kuzindua huduma hii na ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji wa taarifa muhimu na taarifa zinginezo za kwene vyombo vya habari kwa muda muafaka” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Push Observer, Tom Kyalo.

Jumatano, 4 Machi 2015

Jenga uadilifu kwa kupinga rushwa

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kujenga uadilifu kwa kila mtu katika nchi yake, ni kukataa rushwa kwa kutoa au kupokea.

Sefue aliyasema hayo katika Warsha ya Wadau ya kujadili Rasimu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi,Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi iliyoandaliwa na Tume ya Maadili iliyofanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam,alisema wazo la ahadi ya Uadilifu kwa viongozi,watumishi wa Umma na sekta binafsi ni mwanzo wa kampeni kwa nchi nzima.

Alisema sheria kali na adhabu,lakini iwe ni dhamira ya kila mmoja kufuata maadili na kujenga utamaduni wa kutotoa rushwa au kupokea rushwa. Sefue alisema ahadi hizo zitatumika kama muongozo kwa kuzingatia makampuni yaliyotia saini pamoja na viongozi na watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao, hivyo kutachangia katika juhudi za kupambana na rushwa nchini.

Aidha alisema lengo la 3.2 la dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 inayohusu Uongozi bora na utawala wa sheria inakusudia Tanzania kuwa jamii yenye maadili mema ,kuthamini ,utamaduni ,uadilifu,kuheshimu utawala wa sheria na kutokuwepo kwa rushwa na maovu.

Kwa upande wake Kamishina wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu,Salome Kaganda, alisema rasimu ya ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi,Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi ni juhudi za kuunga mkono zilizopo za kukuza uadilifu uwazi na uwajibikaji katika kuimarisha utawala bora nchini.

Salome alisema kuwa walikuwa wakiangaliwa ni watumishi wa umma sasa watahusika sekta binafsi,wanasiasa na wafanyabiashara katika kujenga utawala bora katika nchi.

Source:MICHUZI BLOG

Jumapili, 1 Machi 2015

FAHAMU UMUHIMU WA SAIKOLOJIA YA ELIMU

Unaweza kuwa umeshawahi kusikia neno SAIKOLOJIA mara nyingi sana, Lakini hebu tufafanue zaidi kwa yule ambaye hafahamu maana yake.

Kwa kifupi kwanza hili neno ambalo asili yake ni kigiriki likiwa na maana ya kwamba, saiko ni mambo yanayohusu akili au ubongo, na lojia ni mambo yanayohusu elimu.

Hivyo kwa ujumla tunaweza kusema kwamba saikolojia ni elimu inayohusu mambo ya akili au ubongo. Somo hili la saikolojia linahusu jinsi wanyama na binadamu wanavyoweza kutumia akili au ubongo katika kumiliki na kuongoza vitendo na tabia zao. Ni wazi kuwa wanyama wote wana ubongo Lakini ni binadamu peke yake ndiye mwenye uwezo wa kujifunza kwa kutumia ubongo wake wakati wanyama wengine hujifunza kwa kutumia silika na mazoea. Na hii humfanya binadamu kuwa tofauti na viumbe wengine.

Sehemu kubwa ya saikolojia inahusu jinsi binadamu anavyoweza kutumia ubongo au akili yake katika kujifunza, kufikiri na kudhibiti tabia zake. Kwa ujumla ni kwamba saikolojia ni taaluma ya kisayansi inayohusu tabia/mienendo na michakato ya ubongo au akili ya binadamu katika kujifunza. Tabia au mienendo ni kila kitu ambacho mtu hufanya na ambacho huweza kuchunguzwa moja kwa moja.

Tumeangalia kwa ufupi sana maana halisi ya saikolojia, sasa je unaelewa nini kuhusu saikolojia ya elimu? Kuna matawi mbalimbali ya saikolojia kama vile saikolojia ya Elimu, Saikolojia ya Kliniki, saikolojia ya Biashara, saikolojia ya Kijeshi n.k. hivyo basi katika mada hii tunaangalia maana ya saikolojia ya elimu na umuhimu wake.

Saikolojia ya elimu ni tawi la taaluma ya saikolojia linaloshughulikia masuala ya elimu, tawi hili linachunguza jinsi mwanafunzi anavyojifunza mambo mbalimbali ya kielimu, kijamii na kiutamaduni na namna bora ya kumfundisha. Sasa hebu tuangalie tawi hili lina umuhimu gani? Au kuna umuhimu gani wa mwalimu kujua saikolojia?

Umuhimu wa saikolojia ya Elimu

1. Hii humsaidia mwalimu kujua tabia za mwanafunzi na kujua ni kwa njia au mbinu gani anaweza kuzitumia ili tendo la kujifunza litokee na pia kujua sababu zinazoweza kufanya tendo la kujifunza lisiimarike mfano wanafunzi hutofautiana sana kutokana na malezi waliyolelewa au mahala walipotokea, hivyo kama mwalimu ukishajua tofauti hizi utajua utumie mbinu zipi ili kuhakikisha kuna usawa wa elimu au ulichokifundisha kimeeleweka kwa wote bila ya kubagua mwenye uwezo mkubwa au mdogo.

2. Husadia pia kujua jinsi ubongo au akili ya binadamu inavyotumika katika tendo la kujifunza. Kujua huku kutafufua njia na mbinu mbalimbali kuhakikisha kinachofundishwa kimefanikiwa.

3. Husaidia kumjua vema mwanafunzi wako na kujua jinsi gani utamsaidia ili ajifunze vema zaidi.

4. Itakusaidia kufahamu matatizo yanayokwamisha mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji na kujua jinsi gani utaweza kuyatatua.

5. Kwa kufahamu saikolojia na tabia za wanafunzi wako utaweza kuwaandaa vema na kuwapa motisha ili walipende somo na kuwachochea inapobidi. Mfano unaweza kutumia mifano mizuri ya kile wanafunzi wanachokipenda ili kuwafanya wawe na furaha na umakini na kile unachokifundisha.

6. Utajua kama mwanafunzi ameelewa au hajakuelewa hata kama amekaa kimya bila ya kukuuliza au kusema lolote. Kuna wanafunzi huwa na uoga wa kuuliza swali pale anaposhindwa kuelewa sehemu fulani, hivyo kama una ujuzi wa saikolojia hali hii unaweza kuigundua kwa wanafunzi wako na kuirekebisha.

Kwa upande wangu nina hayo machache, ikiwa una lolote la kuongezea jisikie huru kuacha maoni yako kwani tuko pamoja katika kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali.

Kwa maoni wasiliana nami,
CHACHA,J.Clement
Librarian-Chuo kikuu cha Dodoma
Email:jacksonclement73@gmail.com

Jumanne, 24 Februari 2015

Namna ya kuifanya simu yako idumu na chaji muda mrefu

Ujio wa matumizi ya simu za kisasa maarufu kwa jina la Smartphone umewafanya Watanzania wengi kuzinunua, kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa mawasiliano.

Simu hizi ni sawa na kuwa na kompyuta ya kawaida iliyounganishwa na mtandao wa intaneti. Kwa mfano, simu hizi zinakupa nafasi kubwa ya mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp, Facebook, Skype, Viber, Kik Messenger, Twetter, WeChat, LinkedIn, Badoo, Instagram na Twoo.

Pia simu za kisasa zina huduma mbalimbali zikiwamo za kujua jiografia ya maeneo, vipimo vya joto, mapigo ya moyo, upigaji wa picha na huduma nyinginezo. Kwa kutumia mitandao ya kijamii watu sasa hawana sababu ya kujisika wapweke, kwani hata ukiwa chumbani peke yako unaweza kuungana na watu duniani kwa kujadili na kupokea taarifa mbalimbali.

Hivyo simu hizi zimeweza kuwakusanya watu waliotawanyika sehemu mbalimbali na kujadili mambo kama vile wamekusanyika eneo moja. Mbali na hilo, simu nyingi zina uwezo mkubwa wa kasi ya mawasiliano ya intaneti, hivyo kuwa rahisi kutuma na kupokea barua pepe na kupata taarifa kutoka tovuti mbalimbali duniani. Ni kutokana na mambo hayo, simu hizi zimeonekana ndizo za kisasa na watu wengi wameamua hata kujinyima ili kuzinunua. Kasoro ya simu hizi Pamoja na watu wengi kuzipenda, simu hizi zimekuwa ni kero kutokana na uwezo mdogo wa betri zake kudumu na chaji au nguvu za kuziendesha. Awali watu wengi walipenda simu zinazodumu na chaji muda mrefu. Simu za kisasa zina udhaifu wa kushindwa kudumu na chaji. Nyingi zinatumika kwa saa sita hadi 12. Kwa sababu hii watumiaji wengi wameamua kununua vifaa vya kuhifadhia umeme kwa ajili ya kuzichaji. Vifaa hivi vinajulikana kwa jina la’ power banking’ Kinachokuonyesha kuwa uwezo unapungua ni pale unapojikuta siku za mwanzo unachaji kwa siku moja baadae mara mbili kwa siku, mara tatu na hatimaye unajikuta unachaji mara kwa mara. Kwanini simu hizi hazidumu na chaji kwa muda mrefu kama zilivyo simu nyingine? Nini kifanyike ili kutatua tatizo hili? Wataalamu wana majibu. Sababu za kuisha chaji mapema.

Mmoja wa waanzilishi wa Kampuni ya Farbe Tecnik inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kuchaji simu, Shane Broesky anasema kupungua kwa uwezo wa kuhifadhi chaji kwa simu hizi ni uzembe wa watumiaji. Anasema watu wengi hudhani kuziacha simu zao zikiwa zinachajiwa usiku mzima au kwa muda mrefu ni kupunguza uwezo wa betri kuhifadhi umeme. Broesky, katika maelezo yake aliyoyatoa kupitia mtandao wa Digital Trends, anawatoa hofu wamiliki wa simu kuwa kuziacha kwenye chaji kwa muda mrefu hakuharibu simu zao. Anafafanua kuwa hii ni kwa sababu simu hizo zina mfumo mzuri wa kuzuia umeme usiendelee kuichaji betri baada ya kufikia kiwango cha juu cha asilimia 100. Broesky anasema hii inasaidia kuepusha betri kuchajiwa kupita kiasi. Lakini akasema kitendo cha kuicha kwenye mfumo wa kuchaji, kinasababisha kila betri ikipungua kidogo kutoka kiwango cha juu, ianze kuchajiwa tena. Kitendo hicho kinapojirudiarudia, anasema ndiko kunakoua uwezo wa betri hasa zile za aina ya ‘Lithium-ion’ katika kuhifadhi umeme. Anasema betri hizi zinapokuwa na kiwango cha juu cha umeme, ikichajiwa joto lake linapanda. “Kitendo cha betri kuwa kwenye hali ya joto kwa muda, ndiko kunakoharibu uwezo wake wa kudumu na umeme kwa muda mrefu,’’ anasema. Namna ya kuwezesha chaji kudumu Ili betri ya simu yako iendelee kuwa na uwezo, Broesky anasema unapaswa uichaji kwa kiwango cha kati ya asilimia 50 na 80. Ukitumia mfumo huo, utaifanya betri ya simu yako iendelee kuwa na uwezo wa juu wa kudumu na umeme kwa muda mrefu. Jambo lingine la kuifanya betri yako idumu na umeme ni kuepuka betri yako kupungua umeme hadi simu kuzima. Kampuni ya Simu ya Tecno nayo ilitoa taarifa kwenye mtandao wake kuwa mtumiaji wa simu za kisasa anapaswa kuepuka simu yake kupata moto wakati wa matumizi.

Taarifa ya kampuni hiyo ambayo simu zake zinaonekana kutamba katika soko hapa nchini, inaelezea kuwa iwapo unatumia intaneti katika mazingira ya mawasiliano hafifu, simu hupata moto. Inawashauri watumiaji wa simu hizo pia wasiziache zikiwa zimefunguliwa ukurasa wa mawasiliano ya intaneti kwa sababu wakati mawasiliano yanakuwa madogo, hupata moto.
 
Source:Mwananchi 24,february,2015

Jumatatu, 23 Februari 2015

Kushuka kwa bei ya mafuta kichocheo cha ukuaji wa uchumi:Repoti


Ripoti mpya kuhusu matarajio ya ukuaji wa uchumi duniani ya Benki ya Dunia iliyotolewa hivi leo imesema kufuatia mwaka mwingine wa kukatisha tamaa, nchi zinazoendelea zitashuhudia ukuaji wa kiuchumi mwaka huu, chachu ikiwa ni kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli, ukuaji imara wa uchumi wa Marekani, na viwango vya chini vya riba duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kuongezeka kwa wastani ya asilimia 2.6 mwaka 2014, uchumi wa dunia unatarajiwa kukua kwa asilimia 3 mwaka huu, asilimia 3.3 mwaka ujao na asilimia 3.2 mwaka 2017. Mwaka wa 2014, nchi zinazoendelea zilikuwa kwa asilimia 4.4, lakini mwaka huu zinatarajiwa kuwa kwa asilimia 4.8 na kutabiriwa kukua kwa asilimia 5.3 na 5.4 mwaka 2016 na 2017 mtawalia.

Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim amesema katika mazingira haya ya kubadilika badilika, nchi zinazoendelea zinahitaji kutumia raslimali zake kwa busara katika kuwekeza kwenye miradi ya kijamii kwa kuzingatia watu masikini na kufanya mageuzi ya kimuundo inayowekeza kwa watu.

Ayhan Kose, Mkurugenzi katika Benki ya Dunia. "Hatari ya ahueni hii tete bado ni kubwa. Benki Kuu katika nchi zinazoendelea zinahitaji kuleta usawa kati ya kulenga ukuaji wa kiuchumi na kulenga mfumuko wa bei na utulivu wa fedha. Wakati huo huo, sera ya fedha inaweza kuwa chombo cha kuchochea ukuaji wa uchumi wao, iwapo kutakuwepo na mtikisiko wa kiuchumi.

Jumapili, 22 Februari 2015

KUTENGENEZA PESA KWA NJIA YA INTANETI NA NAMNA YA KUEPUKA KUTAPELIWA

Mtandao wa intaneti umerahisisha karibu kila kitu kwenye maisha yetu. Sasa hivi mtu kwa kuwa na mtandao, na akawa na kompyuta au simu yenye uwezo mkubwa(smartphone) anaweza kuanzisha biashara popote alipo na akiwa na mipango mizuri anaweza kufanikiwa sana.

Mtandao wa intaneti umerahisisha sana ufanyaji wa biashara, kwani kupitia mtandao huu mtu anaweza kutafuta soko la bidhaa au huduma anazotoa. Pamoja na faida hii kubwa ya mtandao wa intaneti, kuna watu wengi ambao wanautumia vibaya kwa kuwatapeli wengine.

Njia zinazotumia kuwatapeli watu kupitia mtandao. Kuna njia nyingi sana ambazo zinatumika kuwatapeli watu kupitia mtandao. Hapa nitazungumzia njia kuu mbili ambazo nimeona wengi wakitapeliwa kwa njia hizo.

1. Kupata mikopo rahisi. Kwenye mitandao ya kijamii, hasa facebook kuna matapeli wanaotumia jina la vicoba saccos. Watu hawa wanaahidi kutoa mikopo rahisi na kwa haraka kupitia njia ya simu. Ili kuwakamata vizuri watu, wamekuwa wakitumia majina ya watu maarufu kusambaza habari hizi. Kwa mfano wanafungua account kwenye facebook kwa jina kama Zitto Kabwe, kisha wanaweka maelekezo kwamba kuna njia rahisi ya kupata mikopo. Kwa watu kuona habari hii inatolewa na mtu wanayemfahamu, inakuwa rahisi kwao kuchukua hatua na hatimaye wanatapeliwa. Watu wengi sana wametapeliwa kwa njia hii. Na pia watu hawa wamekuwa wakitumia majina ya watu wanaojulikanan kwenye jamii na wakati mwingine wanatumia habari maarufu kujiwekea nafasi nzuri ya kuaminika. Matapeli hawa huelekeza watu kwenye tovuti zao ambazo pia sio halisi. Tovuti hizo hukuta zimeishia na neno wapka.mobi, ukiona kitu kama hiki kimbia haraka sana.

2. Aina ya pili ya utapeli ni kufanyishwa kazi ambayo huna uhakika wa kulipwa. Katika aina hii ya pili, hakuna mtu anayekuambia utume fedha, ila wewe unapewa majukumu ya kufanya na pia kuambiwa ushawishi watu wengi wajiunge na kwamba utalipwa kulingana na kazi uliyofanya. Kwa uzoefu wangu mdogo, sijawahi kuona mtu aliyelipwa kwa kazi za aina hiyo. Mifano ya utapeli huu ni link ambazo watu wanashirikishana, unakuta inakuambia pata dola 100 kila siku ukiwa nyumbani. Halafu kazi wanayokupa ni kubonyeza matangazo, na pia kualika wengi zaidi nao wajiunge. Watu wengi wamekuwa wakisambaziana ujumbe wa aina hii wakiamini kwamba jinsi unavyoingiza watu wengi ndivyo unavyopata fedha nyingi, baadae wanapotaka kupata fedha zenyewe ndipo wanagundua kwamba ni utapeli. Ni njia zipi halali unazoweza kutumia kutengeneza fedha kwenye mtandao. Nimekuwa nafanya biashara kwa njia ya mtandao wa intaneti kwa muda sasa.
Na kwa hapa tanzania kuna njia tatu muhimu unazoweza kutumia kujitengenezea kipato cha njia ya mtandao.
1. Njia ya kwanza, kuwa na website, au blog ambayo inatoa taarifa mbalimbali na watu wanaipenda kuifuatilia. Kama ukiwa na watu wengi unaweza kuweka matangazo ya watu wengine na ukalipwa. Unaweza kuweka matangazo ya moja kwa moja kutoka makampuni ya hapa Tanzania au unaweza kujiunga na mpango wa google wa matangazo na wao wakaweka matangazo yao kwenye website/blog yako na wakakulipa kulingana na idadi ya watembeleaji. Njia hii ni rahisi sana na wengi sasa wanaitumia vibaya, kwa mfano kwa sababu watu wengi wanapenda udaku na kuona picha za uchi, basi kuna blog nyingi sana zimeanzishwa zinazotoa habari za udaku na picha za uchi. Jinsi mnavyotembelea wengi ndivyo wanavyopata kipato. Japokuwa hii pia sio njia nzuri ya kuvutia watu kwenye website au blog(kutumia picha za uchi).
2. Njia ya pili ni kuwa na bidhaa au huduma zako mwenyewe na kutumia mtandao kuzitangaza na hata kuziuza moja kwa moja. Kupitia njia hii unakuwa na tovuti au blog ambayo inaeleza kuhusu bidhaa au huduma unazotoa. Watu wanakujua kupitia mtandao na wanakutafuta ili uweze kuwauzia bidhaa au huduma hizo. Kama upo kwenye biashara yoyote ila ni muhimu sana kuwa na blog ambayo itakuwezesha kuwafikia wateja wengi zaidi. Ni njia rahisi sana ya kutangaza na usambaaji wake hauna kikomo.
3. Njia ya tatu ni kuuza bidhaa za wengine. Unaweza kuanzisha tovuti au blog ambapo wewe unakuwa unatangaza na kuuza bidhaa za watu wengine au makampuni mengine. Kwa kiingerea hii inajulikana kama affiliate marketing. Kwa njia hii wewe unachagua bidhaa au huduma ambayo unaona watu wanaihitaji au inaweza kuwasaidia na klisha unawashawishi wainunue. Unaweza kutengeneza kipato kizuri sana kwa njia hii kama ukiweza kuchagua bidhaa/huduma nzuri. Unawezaje kuepuka utapeli kwenye mtandao? Siku moja tapeli mkubwa sana aliulizwa ni mtu gani rahisi kumtapeli, tapeli yule alijibu, ni rahisi sana kutapeli mtu ambaye sio mwaminifu, na ni vigumu sana kumtapeli mtu ambaye ni muaminifu. Kwa kifupi ni kwamba ukiwa mwaminifu hakuna anayeweza kukutapeli. Ila unapokosa uaminifu na kuanza kutafuta njia rahisi za kujipatia fedha(ambazo hazipo) ndio unadondoka mikononi mwa matapeli na wao wanashangilia. Ili kuepuka kutapeliwa kwenye mtandao, zingatia mambo yafuatayo;
1. Hakuna kitu cha bure. Ili upate fedha unahitaji kufanya kazi ambayo itazalisha thamani kwa mtu mwingine. Unapokutana nafursa yoyote ya kutengeneza kipato kwenye mtandao, jiulize je ni thamani gani ambayo natengeneza hapa? Yaani mtu mwingine anafaidika vipi na hiki ninachofanya kwenye mtandao ili kupata fedha. Kama hakuna anayefaidiaka usiingie kwenye biashara hiyo.
2. Hakuna njia ya mkato. Ili kupata kitu unachotaka, hakuna njia ya mkato. Unahitaji kufuata kila hatua muhimu ndio uweze kufikia kile unachotaka. Ukishaanza kutafuta njia za mkato umekwisha, ni lazima utatapeliwa.
3. Hakuna mkopo unaopatikana kirahisi. Njia hii ya mikopo kupitia mtandao imesababisha wau wengi sana kutapeliwa. Labda nikuulize swali, mtu akaja sasa hivi hapo ulipo akakuambia nikopeshe elfu 50 na nitakurudishia, hata kama unayo utamkopesha? Kumbuka huyo ni mtu ambaye humjui, hujui anakwenda kufanya nini na fedha hizo ila anataka umpatie. Mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kumkopesha fedha mtu asiyemjua, tena asiyejua anakwenda kufanya nini na fedha hizo. Ndio maana mabenki na taasisi nyingine wanakuwa na dhamana, ili mkopaji asikimbie.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya kuboresha maisha.

CHACHA,J.Clement
Librarian-The University of Dodoma
E-mail:jacksonclement73@gmail.com

Jumamosi, 21 Februari 2015

INTANETI

Intaneti ni nini?

ni mfumo wa kushirikiana kwa kompyuta unaowezesha kompyuta mbalimbali duniani kuwasiliana kati zao. Kupitia mtandao huu, watu huweza kutembelea tovuti mbalimbali, kupiga gumzo, na kuandikiana barua pepe. Ni ile mawasiliano ya tarakilishi pamoja na habari zinazotunzwa kwenye mashine na kupatikana kwa programu za kutafuta (kama google) au kwa kamusi kama wikipedia.

Intaneti ni mfumo wa ulimwengu wa mitandao ya kompyuta inayotumia Itifaki inayokubalika ya intanet Suite (TCP / IP) kutumikia mabilioni ya watumiaji duniani kote. Ni mtandao wa mitandao ambayo ina mamilioni ya mitandao binafsi, mitandao ya umma, mitandao ya kielimu, mitandao ya biashara, na mitandao ya serikali zenye upana wa kimitaa na kiulimwengu ambazo zimeunganishwa na safu pana ya teknolijia za mtandao za elektroniki na za mwangaza.

Intanet hubeba safu kubwa ya huduma na rasilimali za habari hasa hati za HyperText zilizoshikanishwa za Mtandao wa ulimwengu nzima (WWW) na miundombinu ya kusaidia barua pepe. Mbinu nyingi za jadi za mawasiliano ya habari, kama vile huduma za simu na televisheni, zimeundwa upya kutumia teknolojia za intanet, na kusababisha huduma kama vile itifaki ya kupitisha sauti kwa kutumia intanet (VoIP) na IPTV. Uchapishaji magazeti umeundwa upya katika Tovuti, ubadilishaji maoni, na kupatiana habari zinapotokea. Intanet imewezesha au kuharakisha uumbaji wa aina mpya za mwingiliano za kibinadamu kupitia ujumbe wa moja kwa moja, jukwaa za Intanet na tovuti za kijamii.

Asili ya mtandao ina mizizi katika mwongo wa 1960 wakati Marekani ilifadhili miradi ya utafiti wa wakala zake za kijeshi na kujenga mitandao iliyosambaa ya kompyuta ambazo zina uwezo wa kustahimili mabadiliko na ni vumilivu kwa makosa. Kipindi hiki cha Utafiti na ufadhili wa raia wa Marekani wa uti mpya wa mgongo uliyofanywa na msingi wa kitaifa wa sayansi ulisababisha dunia yote kushiriki katika maendeleo ya teknolojia mpya na ukasababisha ufanya biashara wa mtandao wa kimataifa katikati ya mwongo wa 1990, na kusababisha kujulikana kwa zana nyingi katika karibu kila nyanja ya maisha ya kisasa ya binadamu. Kufikia mwaka wa 2009, wastani wa robo ya idadi ya watu duniani hutumia huduma ya Intanet. Intanet haina utawala wa kati katika utekelezaji wa kiteknolojia au sera ya upatikanaji na matumizi; kila mtandao jumuishi unaweka masharti yake yenyewe. Ufafanuzi tu wa jina mbili kuu katika Intanet, Itifaki ya anwani za Intanet na mfumo wa makundi ya majina, ndizo zinazongozwa na shirika iliyoagizwa ya, Ushirika wa kupeana majina na nambari za intaneti(ICANN).

Msingi wa kiteknolojia na masharti ya itifaki misingi (IPv4 na IPv6) ni shughuli ya kikundi maalum kilichoundwa kutekeleza kazi za uhandisi wa intanet (IETF), ambalo ni shirika la kimataifa lisilo la kutengeza faida ambalo washiriki wanaweza kuhusika nalo kwa kutoa mchango wa kitaalamu.

Kwa msaada wa mtandao
Imetayarishwa na,

CHACHA,J.Clement
Librarian-The University of Dodoma
Email-jacksonclement73@gmail.com

Ijumaa, 20 Februari 2015

FAIDA ZA KUTUMIA TANGAWIZI AU CHAI YA TANGAWIZI

Katika miaka 500 iliyopita tangawizi ilianza kutumika mashariki ya mbali, kama vile China na India wakitumia kwa kutibu maradhi mbali mbali. Katika hili zao la tangawizi kuna vyanzo vya: Mangenisium Mangnese Potasium Copper Vitamini B6 Hii ikiwa katika mwili wa binaadamu ikiwa ni pamoja na ugunduzi wa wataalamu kutengeneza tangawizi ni tiba tosha kwa magonjwa ya ngozi Hili hapa kwenye picha ni zao la tangawizi kama linavyoonyesha likiwa bado kusagwa.
Faida za kutumia tangawizi:
-.Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wnawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.
-Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.
-Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
-Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.
-Husaidi kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.
-Tangawizi husaidia kupunguz maumivu mwilini
-Husaidia kutoganda kwa damu mwilini
-Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu. Husaidi kuponya fluu kwani chai ya tangawizi ni salama Hizi ndizo kazi za Tangawizi kama tiba ya afya yako Tangawizi ina umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu. Sana sana tangawizi hutumika kama kiungo katika mapishi. Manufaa yake kiafya ni kama ifuatavyo. Tumbo: Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula. Aidha tangawizi humuongezea mtu hamu ya kula. Kichefuchefu na Kutapika: Utafiti unaonyesha kuwa tangawizi ni tiba mufti kwa matatizo haya. Aidha huweza kutumiwa kupunguza tapishi inayotokana na uja uzito. Matatizo ya Moyo: Tangawizi huimarisha moyo wa binadamu na kumwepushia maradhi ya moyo. Hii ni kwa kuwa inapunguza kiwango cha mafuta mwilini. Matatizo ya Kupumua: Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali. Maumivu: Huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na shinikizo la mawazo, kisunzi, na kukosa umakini. Maumivu ya Hedhi: Hupunguza maumivu ya wakati wa hedhi. Malaria: Husaidi kutibu Malaria na Homa ya Manjano. Nguvu za Kiume: T angawizi husaidia kuongeza nguvu za kiume kwa kutibu tatizo la mwanamume kutoa shahawa haraka. Figo: Inaaminika kuwa tangawizi inatibu tatizo la vijiwe vya kwenye figo. Nywele: Aidha hutumiwa kutunza nywele, kwa kuwa huondoa uyabisi (Dandruff.) Saratani: Hutumiwa na wataalamu wa kimatibabu katika tiba ya saratani.

Jumatano, 18 Februari 2015

Majambazi yafunga mtaa,yaua mmoja

Matukio ya ujambazi na mauaji ya kutumia silaha, yameanza kuibuka kwa kasi katika maeneo ya  Magu. Matukio ya ujambazi na mauaji ya kutumia silaha, yameanza kuibuka kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini. Hali hiyo imekuwa ikihojiwa na wananchi na wapenda amani na zaidi ni kuhusu intelijensia ya polisi kushindwa kugundua mipango ya uhalifu. Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa kushamiri kwa matukio hayo kunaleta hofu katika jamii huku jamii yenyewe ikilaumiwa kwa kukaa kimya kwa watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na hutumia isivyo halali. Hali hiyo imetokea mjini Magu, mkoani Mwanza kwa watu wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za moto usiku wa kuamkia jana walifunga Mtaa wa Kisesa Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza na kumuua mfanyabiashara Nestory Andrew umbali wa mita 50 kilipo Kituo cha Polisi. Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku, majambazi hayo yalifunga Barabara ya Mwanza-Musoma kwa muda na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Kisesa huku milio ya bunduki ikitawala anga. Wakizungumza na Mwananchi eneo la tukio jana, mashuhuda walisema walianza kusikia milio mizito ya vitu kama bomu na kwamba baada ya muda wakaona watu wakivamia duka la mfanyabiashara huyo na kupiga risasi hewani. Mmoja ya mashuhuda hao, Daud Mwalimu alisema “Mimi ni fundi baiskeli hapa stendi jana (juzi) muda kama wa saa mbili usiku nilisikia sauti ya vishindo kama bomu, lakini baada ya muda nikasikia sauti za bunduki hewani,” Aliongeza: “Kwa kweli tulitawanyika watu wote hapa mtaani na kuacha mali zetu. Baada ya kutulia tulikuja kushuhudia nini kilitokea, lakini tulikuta mtu mmoja ambaye ni mfanyabiashara hapa Kisesa anavuja damu tulimuangalia tukamkuta amefariki.” Shuhuda mwingine, Emmanuel Juke alisema watu hao walifunga Barabara ya Mwanza-Musoma na kwamba, walikuwa wakipiga risasi ovyo hewani. Juke alisema hali ilikuwa mbaya, kwani hawakuwahi kushuhudia tukio kama hilo na mtu aliyefariki alikuwa mfanyabiashara maarufu Kisesa. Mwandishi w habari hizi jana alifika Kituo cha Polisi Kisesa ambako askari wa kituo hicho walikiri kuwapo kwa tukio hilo huku wakitaka atafutwe Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Magu. Kamanda w Polisi Magu, Charles Mkapa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akadai msemaji mkuu ni Kamanda wa Polisi Mwanza. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Robert Mnyandwa alimtaja mfanyabiashara aliyefariki baada ya kupigwa risasi na majambazi hao kuwa ni Nestory Andrew mkazi wa Igoma. Mnyandwa alisema hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba, hata thamani ya mali na fedha zilizoporwa haijajulikana kwani mhusika alifariki dunia. “Ni kweli tukio limetokea jana saa mbili usiku na mtu mmoja ambaye ni mfanyabiashara wa Kisesa alipigwa risasi na kupoteza maisha. Bado hatujamkamata mtu na tunaendelea na uchunguzi,” alisema Mnyandwa. Kufungwa kwa mitaa na majambazi, kumesababisha wafanyabiashara hasa wanaojihusisha na biashara ya fedha kwa mitandao kufunga maduka yao mapema. Wafanyabiashara kadhaa wamekwishauawa ama kuporwa fedha zao kutokana na majambazi hayo kuvamia maduka yao.

Source:http;www.mwananchi.com

Maktaba za umma zinakua kwa haraka nchini China

Maktaba za umma zaendelea haraka nchini China Mradi wa pili wa ujenzi wa Maktaba ya Taifa ya China ulizinduliwa hivi karibuni mjini Beijing. Hii inaashiria kuwa maktaba za umma nchini China, zimeingia katika kipindi kipya cha maendeleo nchini China.Maktaba nchini China zimegawanyika katika aina nne, yaani maktaba za umma, maktaba za idara za sayansi na teknolojia, maktaba za shule na maktaba za mashirika. Hivi sasa kwa jumla nchini China kuna maktaba za umma za ngazi ya wilaya na mikoa 2700. Mradi wa pili wa ujenzi wa Maktaba ya Taifa ya China utagharimu yuan bilioni 1.3. Baada ya mradi huo kukamilika maktaba hiyo itakuwa kituo kikuu cha kuhifadhi vitabu vya Kichina. Mradi huo utamalizika na kuanza kutumika mwezi Oktaba, mwaka 2007. Wakati huo maktaba hiyo ya taifa itakuwa maktaba kubwa kabisa ya umma na yenye huduma za kisasa kabisa nchini China. Uzinduzi wa mradi huo ni dalili ya maendeleo ya haraka ya maktaba za umma katika miaka ya karibuni. Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya Maktaba ya China Bw. Zhan Furui alisema, "Katika miaka ya karibuni serikali imetenga fedha nyingi katika sekta ya utamaduni. Hivi sasa maktaba za umma na majumba mengi ya makumbusho yamejengwa katika mikoa na miji mikubwa. Hali hiyo inamanisha kuwa maktaba za umma zimepanda ngazi mpya ya maendeleo." Kutokana na takwimu za Wizara ya Utamaduni, idadi ya vitabu vilivyopo ndani ya makataba za umma inaongezeka kwa 10% kila mwaka na vitabu ndani ya maktaba za umma kwenye sehemu za mwambao, vinaongezeka hata maradufu kwa mwaka. Kadiri uchumi unavyokua, ujenzi wa miji pia unaendelea haraka. Licha ya maktaba za umma za nganzi ya taifa, mkoa na wilaya, maktaba za umma pia zimetokea ambazo hazikuwepo hapo kabla katika sehemu za makazi. Katibu mkuu wa Taasisi ya Maktaba ya Taifa Bi. Tang Gengsheng alieleza kuwa katika nchi zilizoendelea maktaba kwenye sehemu za makazi ni sehemu muhimu ya utamaduni wa wakazi. China ni nchi inayoendelea, ujenzi wa miji haujakamilika, kazi za kujenga maktaba katika sehemu za makazi bado zina nafasi kubwa ya kuendelea. Alisema, "Maktaba kwenye sehemu za makazi zinalenga maktaba kwenye sehemu za makazi mijini, kwenye mitaa ya makazi na vijijini, Wizara ya Mambo ya Raia inaposukuma mbele maendeleo ya utamaduni wa sehemu za makazi, inazingatia zaidi ujenzi wa maktaba, kwani maktaba hizo ziko karibu zaidi na wakazi. Kama mambo mengine yanavyoendelea, maktaba nchini China pia zimeingia katika kipindi kipya cha ustawi." Ili kuzifanya maktaba za umma zitoe mchango mkubwa zaidi, kuanzia mwishoni mwa karne iliyopita, maktaba nyingi za umma zimeamua mwezi Desemba wa kila mwaka kuwa ni "mwezi wa kusoma". Katika mwezi huo maktaba hufanya mihadhara na kuwafahamisha wasomaji vitabu bora vipya. Licha ya "mwezi wa kusoma", kila mwaka katika "siku ya haki ya kunakili duniani", yaani tarehe 23 Aprili, maktaba za umma hufanya shughuli za kuhamasisha watu kusoma vitabu na kufanya mashindano ya kuandika insha, na kuwavutia watu wengi kwenye maktaba na kuwafahamisha kwamba maktaba ni mahali pa kujielimisha katika maisha yote ya binadamu. Ni kweli kwamba maendeleo ya maktaba katika miaka ya karibuni ni makubwa nchini China, lakini maendeleo hayo yakilinganishwa na nchi zilizoendelea bado yako nyuma sana. Mathalan, idadi ya vitabu vinavyohifadhiwa ndani ya maktaba za umma, hivi sasa ni nakala milioni 500 tu kote nchini China. Idadi hiyo ni ndogo sana kiasi cha kusikitisha, ikilinganishwa na idadi kubwa ya Wachina bilioni 1.3, na maendeleo hayo yanatofautiana sana kati ya miji na vijiji, kati ya sehemu ya mashariki na magharibi. Mkurugenzi wa Taasisi ya Maktaba alipozungumzia matatizo ya maktaba alisema, "Maktaba za umma huwekezwa na serikali, lakini kutokana na sababu fulani fedha hazikutengwa au fedha chache zilitengwa, kwa hiyo maendeleo yanaathirika. Tatizo lingine ni kutokuwa na katiba ya maktaba. Matatizo hayo mawili ni sababu muhimu za kukwamisha maendeleo ya maktaba nchini China. Bi. Tang Gengsheng alisema, ustawi wa huduma za jamii unategemea sana uchumi, kwa hiyo kutokana na jinsi uchumi unavyoendela, maktaba za umma nchini China hakika zitapiga hatua kubwa zaidi katika siku za mbele.

Kwa msaada wa mtandao,
Imeandaliwa na

CHACHA,J.Clement
Librarian-The University of Dodoma
E-mail:jacksonclement73@gmail.   com

UTATUZI WA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA TANZANIA

Vijana wengi wanamaliza vyuo mbalimbali nchini .Changamoto wanazokumbana nazo baada ya kuhitimu masomo yao ni ukosefu wa ajira.Nikasema, labda tuanzishe mjadala mahsusi wa kitaifa, utakaolitazama suala la ajira kwa vijana wa kitanzania kwa mapana na marefu, na kulifanyia utekelezaji. Vijana wa zama hizi hawataki maneno, wanataka vitendo. Maneno na mipango mizuri iliyoandikwa haitowasaidia sana, wanahitaji fursa za ajira, za kujiajiri, za kuendesha maisha yao. Tena vijana wa siku hizi hawako tayari kutumiwa na wanasiasa kwa faida za kisiasa. Hii ni Tafakuri Tunduizi yangu juu ya ufumbuzi wa tatizo la ajira kwa vijana na pia kukuza uchumi wa nchi yetu. haimaanishi hii ndiyo kila kitu na kwamba lazima vijana wote watataka kuwekeza kwenye industry nilizozitaja hapa, hii ni dira tu; Tuanzishe mfuko maalum wa kutoa mikopo ya uwekezaji kwa vijana wa kitanzania. Mfuko huu utawalenga vijana watakaowekeza kwenye sekta ambazo tutazichagua, sana sana tutoe kipaumbele kwenye sekta za kilimo na viwanda vyenye backward au forward linkage na kilimo, moja kwa moja. Vijana hawa waingizwe kwenye challenge ya kupata mikopo, ambayo itatakiwa iwe na masharti nafuu, iwe na riba ndogo (asimilia 8 kushuka chini), iwe na payback period ndefu, ya miaka 15-20, isiwe na masharti ya dhamana/security za mali (maana vijana hawana assets zozote!) bali iwe na dhamana nafuu kama cheti cha elimu ama ardhi (shamba lililorasimishwa). Mpango huu uendane na kutengeneza utaratibu mzuri na rahisi wa kusajili mashamba. Yatengwe maeneo maalum ya kuwekeza. Vijana wawe guided kuwekeza kwenye sekta zilizochaguliwa na wawezeshwe kupata mitaji hiyo. Kama tutakuwa na vijana wataowezeshwa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda kama vya kuchambua pamba, kukoboa na kusaga unga/chakula cha mifugo, kukamua na kusafisha mafuta ya kula, pia kutengeneza sabuni, kusindika juice, viwanda vya nyuzi (spinning mills), tutaweza kuwataka wawekezaji hawa vijana kuhamasisha kilimo cha kisasa na kusupport wakulima kwenye maeneo yao (linaweza kuwa sharti mojawapo la kupata mikopo hii maalum kwa ajili ya vijana) kwa kuwa-supply farm inputs, farm machinery, improved seed varieties etc – hii itasaidia kuongeza tija na ufanisi kwa wakulima. Pamoja na kuongeza tija na ufanisi (productivity and efficiency), tutakuwa tumeongeza volume of farm and industrial produces (uzalishaji), uhakika wa soko utakuwepo (market stability and sustainability) na hatutouza mazao fresh kutoka shambani bali tutauza finished goods au semi-processed goods ambazo zimefanyiwa value addition kwenye viwanda vyetu; finally tutakuwa tumetatua tatizo si tu la ajira bali hata la kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao yetu, kuhakikisha masoko ya uhakika kwa wakulima wetu na mwishowe kupunguza inflation ya vitu na zaidi zaidi kuongeza exports na kupunguza imports kitu ambacho kitasaidia ku-stabilise our BOP (balance of payments) account. Hapa pia tutakuwa tumetatua tatizo la kuanguka thamani kwa shilingi yetu. Ukiongelea kuimarisha uchumi wa nchi basi ni lazima uongelee kuongeza tija na ufanisi ambao utaongeza uzalishaji na ubora wa bidhaa zenu, na wala siyo austerity measures za muda mfupi zinazopelekea kuimarisha fedha na viwango vyetu vya exchange rate against other foreign currencies. Ukiuangalia mpango huu utagundua kwamba kutakuwa na vijana wasomi (watakaoandaliwa kuwekeza kwenye viwanda) na wale ambao hawajasoma (watakaowekeza kwenye kilimo), haya makundi yatabebana – kwenye model hii, na hivyo kila kundi litatoa ajira kwa watu wengi zaidi. Kwa nini basi mimi hapa napendekeza mikakati hii iwalenge vijana? Vijana, tukiondoa factors nyingine, kibaiolojia tunawategemea bado watakuwepo kuwepo hapa duniani kwa muda mrefu kidogo kuliko makundi mengine, na hivyo kama tutaendelea kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi hii ndogo na usiwaowashirikisha vijana kwa maksudi, maana yake wataishi maisha yao yote ya ujana, ujuzi, nguvu na ndoto kwa shida sana bila kutumika ipasavyo. Pia, ili kuwa na uchumi imara, ni lazima tujipange kwa kuangalia mbali kidogo, siyo kwamba tunafanya nini leo ili tufanikiwe leo! Tukiwatumia vijana kwa kuona mbele, wakiwekeza leo na wafanikiwa kuendesha biashara zao kwa faida maana yake ni kwamba baada ya miaka 20, Tanzania itakuwa na matajiri wengi zaidi, na itatoka kwenye kundi la nchi za daraja la tatu! Pia, ni rahisi sana kwa kijana kuchukua risk na kufanya kazi kwa bidii kufikia ndoto zake bila wasiwasi, na zaidi kundi hili likopewa kipaumbele linaweza kuibadili kabisa culture ya watanzania kutoka kwenye ‘business as usual’ na ‘laissez-faire’ na kuwa nchi ya watu wenye kufanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu na passion ya ukweli. Mimi naliona hili ndiyo kundi pekee litakaloweza kuijenga Tanzania mpya, Tanzania ya miaka 20 ijayo… haimaanishi wazee ‘wa busara’ wasiwepo kabisa, hapana lakini kwenye mpango huu wa kujenga upya viwanda vyetu na kutoa ajira kwa vijana, wasihusike. Ni lazima tuwe na ndoto. Ni pia ni lazima tujipange kuzifikia ndoto zetu. Hakuna ujanja mwingine. Hatuwezi kufanikiwa kwa kutumia mikakati ile ile iliyotufikisha hapa. Huwezi kupanda mchicha ukajiandaa kuvuna bangi! Tunahitaji kubadilika, tunahitaji new approaches, new ideas… tukiwa na new approaches sasa hapo tunaweza kuona new results!

Imeandaliwa na
CHACHA ,J.Clement
Librarian-University of Dodoma

Chanzo :http://www.mwanabidii.com Source: http://www.mwanabidii.com

Jumatatu, 16 Februari 2015

TAHARUKI:Maswali 10 uvamizi Tanga

Tukio la kurushiana risasi kati ya polisi wakishirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Askari wakiwa kwenye mapango ya Amboni Tanga juzi walipokuwa wakiwasaka watuhumiwa.
Tukio la kurushiana risasi kati ya polisi wakishirikiana na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) dhidi ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi au magaidi limeacha maswali 10 muhimu yanayolifanya lionekane lenye utata. Mpaka sasa hakuna taarifa za kina juu ya tukio hilo lililotokea siku nne zilizopita na kusababisha kifo cha mwanajeshi na wapiganaji wengine zaidi ya sita ambao hawajajulikana kujeruhiwa. Jana katika mkutano wake na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula alijaribu kujibu baadhi ya maswali hayo ambayo yamewafanya wananchi wa Tanga na mikoa mingine nchini, kupata taharuki na kufananisha tukio hilo na matukio ya kigaidi yanayotokea katika nchi mbalimbali duniani. Hata hivyo, majibu ya Magalula, kama ilivyokuwa katika taarifa ya awali iliyotolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, yaliwaacha waandishi wa habari na maswali mengi kuliko majibu, kwani mbali na kuwatoa hofu wananchi, kuna maswali aliyajibu kwa kifupi bila ufafanuzi wa kutosha, hivyo kuzidi kulifanya tukio hilo kuwa na utata. Swali la kwanza ambalo wananchi wanajiuliza ni iwapo tukio hilo ni la kigaidi au ujambazi? Akijibu swali hilo na kukataa kuulizwa swali la aina hiyo tena, Magalula alisema tukio hilo ni la ujambazi. Kauli ya mkuu huyo wa mkoa inafanana na ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe ambaye juzi aliliambia gazeti hili kuwa tukio hilo ni la uhalifu wa kawaida. Alisema polisi wanafahamu kuwa kuna hali ya hatari na wameshaongeza ulinzi katika maeneo yote, kwamba juhudi zaidi zinaendelea kufanyika ili kulinda usalama wa raia na kuifanya Tanzania ibaki kuwa kisiwa cha amani. Swali la pili, waliohusika katika mashambulizi hayo ni raia wa nchi gani? Magalula alisema swali hilo halina majibu na kwamba majibu yake yatapatikana baada ya kukamatwa kwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Juzi, Kamishna Chagonja alikaririwa akisema mapigano hayo yalifanyika katika msako wa majambazi walioiba silaha kwenye kituo cha polisi mkoani Tanga, huku taarifa nyingine zikisema mmoja wa watuhumiwa tayari alikuwa mikononi mwa polisi. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi Makosa ya Jinai nchini (DCI), Diwani Athumani alisema matukio ya uhalifu yanayotokea nchini ni mapya na yanayochochewa na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano. Swali la tatu ni iwapo wahalifu hao waliuawa katika mashambulizi au walitoroka na walipita wapi? Katika majibu yake Magalula alisema hakuna mwili wowote ulioonekana au kuokotwa na operesheni ya kuwasaka bado inaendelea. Swali la nne, ni juu ya eneo la Amboni yalipotokea mashambulizi kama lina mapango yanayoishia mkoani humo au yanatokezea hadi nchi jirani kama inavyodaiwa? Pamoja na Magalula kusema kuwa kuna simulizi nyingi ambazo hazina uhakika juu ya pango hilo, mkazi mmoja wa eneo hilo ambaye hufanya kazi ya kupiga picha alisema eneo la Amboni lina jumla ya mapango 13 yaliyogunduliwa lakini yanayotumika ni mawili. Mapambano yamefanyika katika pango la mbali na lile linalotembelewa na wageni. Swali la tano, ni juu ya waliojeruhiwa katika tukio hilo? ADVERTISEMENT Magalula alisema waliojeruhiwa ni askari wa JWTZ na polisi na wamelazwa katika hospitali ya Bombo, lakini hadi sasa hawajatajwa majina. Mbali na maswali hayo, pia wananchi wanajiuliza maswali mengine ambayo ama hayajapata majibu au majibu yake hayajawaridhisha, kama vile, Je, lengo la uvamizi lilikuwa nini, mtuhumiwa aliyekuwa anashikiliwa na polisi alitorokaje, je, alikuwa amefungwa pingu na iwapo sasa kuna uhakika wa usalama? Maelezo ya ziada Akitoa maelezo zaidi juu ya tukio hilo, RC Magalula alisema hadi jana mchana hakukuwa na mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Alisema kufuatia hali hiyo, maofisa wa vikosi vya ulinzi na usalama wameahamia kwenye mapango mengine ili kujiridhisha kama wahalifu hao watakuwa wamejificha huko. “Kama inavyofahamika eneo la Amboni lina mapango zaidi ya 13, hili lililofanyiwa mashambulizi liko umbali wa kilomita tano kutoka lile linalotumika kwa utalii, kwa hiyo ili kujiridhisha ni lazima maofisa wakague sehemu zote,” alisema Magalula. Mkuu huyo wa mkoa alisema hali sasa imerejea kuwa shwari na amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao. Alipotakiwa na waandishi wa habari kufafanua kwanini aseme hali ni shwari wakati hakuna hata jambazi aliyekamatwa wala silaha zilizotumika kuwashambulia askari akiwamo Sajenti Said Kajembe aliyeuawa, Magalula alijibu kwa kifupi kuwa ni kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vimeshatafuta kila pembe ya Tanga na kujiridhisha. “Serikali ina mkono mrefu imeshatafuta kila pembe ya Tanga na imejiridhisha kwamba hali ni shwari na ndiyo maana nipo hapa kuwaeleza wananchi waendelee na kazi zao,” alisema Magalula. Eneo la utalii Kuhusu eneo la utalii la mapango ya Amboni, Magalula alisema halikuguswa wala wahalifu hawakuwa wamejificha huko na ndiyo maana shughuli za kuwapokea na kuwatembeza wageni zilikuwa zikiendelea. Mwananchi ilikwenda katika lango kuu la mapango ya utalii ya Amboni ambako mhifadhi mkuu, Jumanne Gekora alisema tukio la mashambulizi limeathiri shughuli za mapango hayo. Mhifadhi huyo aliviomba vyombo vya habari viifahamishe jamii kwamba sehemu iliyoshambuliwa si hapo kwenye utalii bali ni umbali wa zaidi ya kilomita tano na ni mapango ambayo hayapo hata kwenye utaratibu wa kuwatembeza wageni. Hospitalini Bombo Habari kutoka hospitalini walikolazwa majeruhi watano ilielezwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri ingawaje bado waandishi wa habari hawajaruhusiwa kwenda kuwaona na hawakutajiwa majina yao. Wakati huohuo askari aliyeuawa katika mashambulizi hayo,Sajent Said Kajembe (47) wa kikosi cha 37 JWTZ amezikwa leo katika kijiji cha Bungu kata ya Dindira Wilayani Korogwe akiwa ameacha mjane na watoto watatu. Mdogo wa marehemu, Bakari Kajembe alisema familia yao imepokea kwa masikitiko kifo hicho kwa sababu Sajenti Said alikuwa tegemeo kwao kutokana baba yao kufariki dunia miaka ya nyuma.

KILIMO CHA KISASA CHA MAHINDI

Mahindi ni chakula muhimu na ni aina ya nafaka katika mataifa ya Afrika yaliyomo kusini mwa jangwa la Sahara. Ni chakula cha matumizi ya nyumbani kwa idadi ya watu inayokadiriwa kuwa asilimia 50. Ni chanzo muhimu cha madini na kuongeza nguvu mwilini, protini, madini ya chuma (iron) vitamini na madini mengine asilia.Waafrika hutumia mahindi kwa njia mbalimbali – (uji, ugali na pombe). Na mahindi ya kuchoma. Kila sehemu ya mmea wa mahindi ina thamani kiuchumi : punje, majani, shina na magunzi huweza kutoa kiasi kikubwa cha bidhaa nyinginezo zilizo chakula na zisizokuwa chakula. Vile vile mahindi ni chakula muhimu cha mifugo (ng’ombe) na huhifadiwa kama silage. Pia mabaki ya mimea na nafaka na pia hutumika viwandani kutengeneza wanga na mafuta. Mahitaji ya mahindi katika hali ya hewa, udongo na Mahindi ni mimea ambayo hustahimili mabadiliko mengi ya hali ya hewa na humea katika maeneo mengi tofauti. Kuna aina nyingi za mahindi yanayotofautiana katika muda wa kukomaa, mahindi huwa na ustahimili mkubwa kwa mabadiliko katika kiwango cha joto. Mahindi haswa huwa mimea ya maeneo ya joto ambako unyevu ni wa kutosha. Mmea huu unahitaji kiwango cha joto cha kila siku cha nyuzi joto 20º ili umee vyema. Joto la juu sana kwa mazao mazuri ni kama nyuzi joto 30º. Hupandwa sana katika sehemu zilizo katika kimo cha mita 3000 kutoka bahari hadi kwenye ukanda wa pwani. mahindi yaweza kupandwa kama chakula cha mifugo.
Mahindi huwa yanaathirika na ukosefu wa unyevu wakati wa kutoa maua na matunda. Pia yanahitaji maji ya kutosha wakati wa kupanda. Katika nchi za joto jingi (tropiki), mahindi hufanya vyema katika mvua ya kiwango cha milimita 600 hadi 900 wakati wa kukua. Mahindi yanaweza kukuzwa kwenye aina nyingi za udongo lakini hukua vyema zaidi katika mchanga, usiotuamisha maji mengi, ulio na hewa ya kutosha na ulio na rutuba na madini ya kutosha. Kuwepo kwa mazao mengi ya mahindi kunapelekea kunyonywa sana kwa madini kwenye udongo. Mahindi yaweza kukuzwa katika udongo ulio na hali ya mchanga na (PH) kutoka 5 hadi 8 ingawa 5.5 hadi 7 ndio mwafaka. Mahindi yako katika kikundi cha mimea kinachoaminika kuathirika na hali ya chumvi katika maji na udongo. Kwa vile mimea ambayo ni michanga huwacha sehemu kubwa bila kuzingirwa na ardhi, mmomonyko wa udongo na kupoteza maji hutokea sana sana hivyo basi ni bora umakini uzingatiwe katika uhifadhi wa udongo na maji kwa kuweka matandazo (mulching).

MATUMIZI YA MBOLEA
Mahindi hustawi zaidi yakiwekwa mbolea, iwapo mambo mengine yanayosaidia katika kukua pia yapo kwa kiwango kinachostahili. Mbolea inayotumiwa na wakulima wadogo mara yingi huwa haitoshi. Mahindi ya kiwango cha juu yaweza tu kufikia kiwango cha juu cha Uzalishaji iwapo yatapewa lishe na madini ya kutosha. Mahindi ya tani 2 kwa hekta na tani 5 kwa hekta hutumia karibu kilo 60 N, kilo 10 za P205 na kilo 70 K20 kutoka katika udongo. MAhindi hunyonya Nitrogen pole pole katika miezi ya kwanza baada ya kupanda, lakini huongezeka hadi kiwango cha juu kabisa wakati wa kutoa maua na kukuza tunda (gunzi). Mahindi huhitaji nitrogen kwa kiwango cha juu na ukosefu huwa ndio kizingiti. Kiwango cha juu cha nitrogen kinahitajika mara tatu; kwanza wakati wa kupanda, pili, wakati ambapo mmea umefikia sentimita 50 za urefu na tatu, wakati matunda ya mahindi yanaanza kutoa zile nyuzi nyuzi nyororo (silking). Udongo mwingi huwa na madini ya phosphorous (P205) na potassium (K20) lakini sio kiwango kinachotosheleza mahitaji haswa ya mbegu za mahindi zinapochipua. Nyunyuzia P205 karibu na mbegu ili ziote kwa haraka. K20 hutumika kwa kiwango kikubwa lakini hitaji la mimea hubainika baada ya upimaji wa hali ya udongo kujua kiasi cha mahitaji (soil test).

DALILI ZA UPUNGUFU WA MBOLEA

Ukosefu wa K20 husababisha ncha za majani kuwa na rangi ya njano na kuunda gunzi (cob) lisilo na punje hadi juu. Ukosefu wa P205 hufanya matawi kuwa na rangi ya samawati na mbegu zisizo laini. Dalili za ukosefu wa nitrogen ni majani ya rangi ya manjano na mimea dhaifu mifupi. Phosphate haifyonzwi haraka na mahindi na pia udongo mwingi wa nchi za joto hukosa madini hayo ya phosphate. Inashauriwa unyunyuzie mbolea ya kiasili kama samadi kabla ya kulima ili uboreshe hali ya udongo na kuongezea madini. Katika ukulima wa kiasili, (organic farming, Nitrogen (N) hutiwa kwenye udongo kupitia kwa upandaji wa mimea ya jamii ya mikunde (legumes) ambayo hutoa nitrogen katika hewa, Hata hivyo mapendekezo ya kimbolea yaliyo katika misingi ya uchunguzi wa udongo hutoa nafasi nzuri ya kupata kiasi kizuri cha mbolea bila kuweka kiwango cha chini au juu. Omba msaada kutoka kwa mafisa ugani wa kilimo waliyo katika eneo lako. Katika maeneo yanayo tegemea mvua kukuza mahindi, panda mbegu wakati wa mvua ya kwanza. Hii itaruhusu mizizi kunyonya madini yaliyotengenzwa na bakteria katika udongo. Maji yaliyosimama huyeyusha na kuondoa madini ya nitrogen kutoka katika udongo na kusababisha ukosefu wa Nitrogen.

KUDHIBITI MAGUGU

Udhibiti wa magugu ni muhimu sana. Katika wiki 4 hadi 6 za mbele baada ya kumea, mahindi huathiriwa sana na magugu. Ni lazima mahindi yapandwe mara moja baada ya kutayarisha shamba. Unaweza kulima katikati ya laini za mahindi ili udhibiti magugu. Nchini Tanzania, kupalilia mara mbili kunahitajika kwa aina nyingi za mahindi, ingawa kupalilia kwa mara ya tatu kutahitajika kwa aina ambazo zinahitaji miezi 6 hadi 8 kukomaa. Kupalilia kwa mikono kunahitaji siku 15 kwa hekta la mikono (power tiller) ni masaa mawili mpaka matatu kwa ekari.

UHUSIANO WA NIPE NIKUPE Desmodium (desmodium uncinatum) nyasi ya Molasses (melinis minutifolia) zikipandwa kati kati ya laini za mahindi huzuia wadudu kama stalk borers moths. Mimea hii hutoa kemikali ambazo huwafukuza wadudu aina stem borers’ moths. Zaidi ya hayo Desmodium huzui gugu haribifu,witchweed striga hermonthica. Napier grass (pennisetum purpureum) na Sudan grass (sorghum vulgare sodanese) ni mimea mizuri sana inayonasa wadudu aina ya stem borers. Napier grass ina njia yake madhubuti ya kujikinga dhidi ya wadudu wanaotoboa mmea kwa kutoa utomvu kutoka kwenye shina, ambayo huzuia wadudu kufyoza mmea na kusababisha uharibifu. Nyasi hizi pia huvutia adui wa stem borers kama mchwa, earwigs na buibui. Nyasi aina ya Sudan pia husaidia maadui asilia, kama nyigu (parasitic wasp)

MAHINDI TAYARI KWA KUVUNWA

Mahindi huweka kivuli kwenye mimea ya mboga mboga ikipandwa safu moja katikati ya mboga kwenye maeneo yaliyo na jua kali. Hii huongeza mazao ya mboga zilizopandwa hivi. na mimea jamii ya mikunde huongeza nitrogen kwenye udongo ambayo huitajika zaidi katika ukuaji wa mahindi pia hupunguza wadudu aina ya (leafhoppers, leafbeatles, stalk borers na fall army worm), upandaji wa mimea jamii ya mikunde ufanyike mara baada ya palizi ya kwanza

KUPUKUSUA MAHINDI KWA KUTUMIA MASHINE YA MKONO UVUNAJI

Uvunaji hufanyika kwa kutumia mikono kwa mashamba madogo na mashine (combine harvester) hutumika kwa ajili ya mashamba makubwa, Zao la wastani la mahindi ulimwenguni mnamo mwaka 2000 lilikuwa kilogramu 4255 kwa kila hekta. Zao la wastani nchini Marekani ilikuwa kilo 8600 kila hekta, huku mataifa yaliyo chini ya jangwa la Sahara la Afrika yakivuna kilo 1316 kwa kila hekta ya shamba. Zao la wastani katika taifa la Tanzania kati ya mwaka 2001-2005 lilikuwa kati ya gunia 15-19 kwa hekta (sawa na kilo 1350-1750) Ukilima kwa kuzingatia ukulima wa kisasa na kanuni zake kwa Tanzania utavuna kilo 5000 kwa hecta (ukanda wa pwani) na kilo 7500 kwa nyanda za juu kama Iringa, Mbeya, Ruvuma, Arusha n.k

Kwa msaada wa mtandao taarifa imeandaliwa na,

CHACHA,J.Clement
Librarian-The University of Dodoma
E-mail: jacksonclement73@gmail.com

FOREVER LIVING PRODUCT

Kwa afya njema tumia bidhaa za aloe vera kutoka  kampuni ya forever living.Bidhaa tulizonazo ni aloe vera gel ambayo husaidia kuondoa sumu mwilini,maradhi ya kisukari,kuongeza nguvu na mengine mengi.kwa maelezo ya bidhaa nyingine kutoka forever living wasiliana 0769330521

Hali tete nchini

Inavyoelekea kwa sasa amani yetu imeanza kupotea kutokana  na mfululizo wa matukio ya uharifu ikiwamo kuvamiwa vituo vya polisi,kuuawa kwa polisi na jingine kubwa la juzi la mapigano baina ya polisi wakisaidiana  na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) dhidi ya makundi yanayodhaniwa kuwa ni ya kigaidi au ujambazi.

Matukio hayo yanafanya Taifa kuwa katika wasiwasi hasa kwa kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa oktoba na kura ya maoni ya katiba pendekezwa.

Tukio la Tanga
hivi karibuni kumetokea mfululizo wa milio ya risasi zikirindima maeneo ya Tanga kwa zaidi ya saa 48.

Katika mapambano hayo ,askari mmoja wa JWTZ alipoteza maisha na wengine wapiganaji zaidi ya sita wakijeruhiwa.
Mpaka tunaandaa taarifa hii hakukuwa na taarifa ndani ya jeshi kuhusiana operesheni hiyo.

Mbali na kutokamatwa kwa watu hao ambao hawajulikani ni waalifu wa aina gani.

Jumapili, 15 Februari 2015

Umuhimu wa maktaba

Maktaba ni mkusanyiko wa nyaraka mbalimbali zenye taarifa ambazo zimepangiliwa ktk mfumo mzuri .
Maktaba zimegawanyika katika aina nne.kuna maktaba za umma,vyuo na shule sekondari na msingi,maktaba maalumu na maktaba binafsi.
Umuhimu wa maktaba
-Kuelimisha
-Kuburudisha
-kuonya na kuadabisha nk.
  

Imeandaliwa na
CHACHA,J.Clement
Librarian-UDOM university